14 Basi sasa, tazama, ninakwenda kwa watu wangu; haya, nitakuarifu mambo ambayo watu hawa watakayowatenda watu wako siku za mwisho.
15 Akatunga mithali yake akasema,Balaamu mwana wa Beori asema,Yule mtu aliyefumbwa macho asema,
16 Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu,Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu.Yeye aonaye maono ya Mwenyezi,Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho,
17 Namwona, lakini si sasa;Namtazama, lakini si karibu;Nyota itatokea katika YakoboNa fimbo ya enzi itainuka katika Israeli;Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu,Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.
18 Na Edomu itakuwa milkiSeiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake;Israeli watakapotenda kwa ushujaa.
19 Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo,Atawaangamiza watakaobaki mjini.
20 Kisha akamwangalia Amaleki, akatunga mithali yake, akasema,Amaleki alikuwa ni wa kwanza wa mataifa;Lakini mwisho wake atafikilia uharibifu.