27 ukagawanye nyara mafungu mawili; kati ya watu waliozoea vita, waliotoka nje waende vitani, na huo mkutano wote;
28 kisha uwatoze hao watu wa vita waliotoka kwenda vitani sehemu kwa ajili ya BWANA; mmoja katika mia tano, katika wanadamu, na katika ng’ombe, na katika punda, na katika kondoo;
29 twaa katika nusu yao, ukampe Eleazari kuhani, kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.
30 Na katika hiyo nusu ya wana wa Israeli utatwaa mmoja atakayetolewa katika kila hamsini, katika wanadamu, na katika ng’ombe, na katika punda, na katika kondoo, maana, katika wanyama wote, ukawape Walawi, hao walindao ulinzi wa maskani ya BWANA.
31 Musa na Eleazari kuhani wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa.
32 Basi masazo ya hizo nyara walizotwaa watu wa vita, zilikuwa ni kondoo mia sita na sabini na tano elfu,
33 na ng’ombe sabini na mbili elfu,