45 na punda thelathini elfu, na mia tano,
46 na wanadamu kumi na sita elfu;)
47 na katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, Musa akatwaa mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, wa binadamu na wa wanyama, akawapa Walawi, waliolinda ulinzi wa maskani ya BWANA; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
48 Na majemadari waliokuwa juu ya elfu elfu za hiyo jeshi, na maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, wakamkaribia Musa;
49 wakamwambia Musa wakisema, Sisi watumishi wako tumefanya jumla ya hesabu ya watu wa vita walio chini ya mikono yetu, na hapana hata mmoja aliyetupungukia.
50 Nasi tumeleta matoleo ya BWANA, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za muhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya BWANA.
51 Musa na Eleazari kuhani wakapokea kwao hiyo dhahabu, maana, vile vyombo vyote vilivyofanyizwa.