1 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma maragoni, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya wafu;
3 mtawatoa nje wote, waume kwa wake, mtawaweka nje ya marago; ili wasiyatie unajisi marago yao, ambayo mimi naketi katikati yake.
4 Wana wa Israeli wakafanya vivyo, wakawatoa na kuwaweka nje ya marago; kama BWANA alivyonena na Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.
5 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,