1 Ilikuwa siku hiyo Musa alipokwisha kuisimamisha maskani, na kuitia mafuta, na kuitakasa, na vyombo vyake vyote, na hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na kuvitia mafuta, na kuvitakasa;
2 ndipo wakuu wa Israeli, vichwa vya nyumba za baba zao, wakatoa matoleo; hao ndio wakuu wa kabila, hao ndio waliokuwa juu yao waliohesabiwa;
3 nao wakamletea BWANA matoleo yao, magari sita yenye mafuniko juu, na ng’ombe kumi na wawili; gari moja kwa wakuu wawili wawili, na ng’ombe mmoja kwa kila mkuu; nao wakayasongeza hapo mbele ya maskani.
4 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
5 Pokea mikononi mwao, ili kwamba viwe vya kutumiwa katika utumishi wa hema ya kukutania; nawe utawapa Walawi vitu hivyo, kila mtu utampa kama utumishi wake ulivyo.
6 Basi Musa akapokea hayo magari, na ng’ombe, akawapa Walawi.