35 Hakika yangu hapana mmoja miongoni mwa watu hawa wa kizazi hiki kibaya atakayeiona nchi hiyo nzuri, niliyowaapia baba zenu kuwapa,
36 isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, huyo ataiona; nami nitampa yeye na watoto wake nchi hiyo aliyoikanyaga; kwa kuwa amemfuata BWANA kwa kila neno.
37 Na BWANA alinikasirikia mimi kwa ajili yenu, akasema, Wala wewe hutaingia humo;
38 Yoshua mwana wa Nuni asimamaye mbele yako ndiye atakayeingia; mtie moyo; kwa kuwa yeye atawarithisha Israeli.
39 Tena, wadogo wenu, mliosema watakuwa mateka, na wana wenu, wasiokuwa leo na maarifa ya mabaya wala mema, ndio watakaoingia, nao ndio nitakaowapa, nao wataimiliki.
40 Na ninyi basi geukeni, mshike safari yenu, mwende jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu.
41 Ndipo mkanijibu, mkaniambia, Sisi tumefanya dhambi juu ya BWANA, tutakwea kupigana kwa mfano wa yote tuliyoamriwa na BWANA. Mkajifunga kila mtu silaha zake za vita, mkafanya wepesi kukwea mlimani.