7 Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang’a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;
8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
9 Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula;
10 na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.
11 Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.
12 Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu;
13 na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake;