11 Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema,
12 Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini;
13 na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali.
14 Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu,
15 Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.
16 Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
17 Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.