25 Nami nakuomba nivuke, nikaione hiyo nchi nzuri iliyoko ng’ambo ya Jordani, mlima ule mzuri, na Lebanoni.
26 Lakini BWANA alikuwa amenikasirikia kwa ajili yenu, asinisikize; BWANA akaniambia, Na ikutoshe, usinene nami zaidi jambo hili.
27 Kwea katika kilele cha Pisga ukainue macho yako upande wa magharibi, na kaskazini, na kusini, na mashariki, ukatazame kwa macho yako, kwa maana huuvuki mto huu wa Yordani.
28 Lakini mwagize Yoshua umtie moyo mkuu, umtie na nguvu; kwani ndiye atakayevuka mbele ya watu hawa, na nchi utakayoiona atawarithisha yeye.
29 Basi tukakaa katika bonde lililoelekea Beth-peori.