21 Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu;Wamenikasirisha kwa ubatili wao;Nami nitawatia wivu kwa wasio watu,Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.
22 Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu,Unateketea hata chini ya kuzimu,Unakula dunia pamoja na mazao yake,Unaunguza misingi ya milima.
23 Nitaweka madhara juu yao chunguchungu;Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe;
24 Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto,Na uharibifu mkali;Nitawapelekea meno ya wanyama wakali,Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini.
25 Nje upanga utawafifilizaNa ndani ya vyumba, utisho;Utaangamiza mvulana na msichana,Anyonyaye pamoja na mwenye mvi,
26 Nalisema, Ningewatawanyia mbali,Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu;
27 Isipokuwa naliogopa makamio ya adui,Adui zao wasije wakafikiri uongo,Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka,Wala BWANA hakuyafanya haya yote.