22 Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu,Unateketea hata chini ya kuzimu,Unakula dunia pamoja na mazao yake,Unaunguza misingi ya milima.
23 Nitaweka madhara juu yao chunguchungu;Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe;
24 Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto,Na uharibifu mkali;Nitawapelekea meno ya wanyama wakali,Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini.
25 Nje upanga utawafifilizaNa ndani ya vyumba, utisho;Utaangamiza mvulana na msichana,Anyonyaye pamoja na mwenye mvi,
26 Nalisema, Ningewatawanyia mbali,Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu;
27 Isipokuwa naliogopa makamio ya adui,Adui zao wasije wakafikiri uongo,Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka,Wala BWANA hakuyafanya haya yote.
28 Maana hawa ni taifa wasio shauri,Wala fahamu hamna ndani yao.