39 Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye,Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi;Naua Mimi, nahuisha Mimi,Nimejeruhi, tena naponya;Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,
40 Maana, nainua mkono wangu mbinguni,Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele,
41 Nikiunoa upanga wangu wa umeme,Mkono wangu ukishika hukumu,Nitawatoza kisasi adui zangu,Nitawalipa wanaonichukia.
42 Nitailevya mishale yangu kwa damu,Na upanga wangu utakula nyama;Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara,Katika vichwa vya wakuu wa adui.
43 Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake;Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake,Atawatoza kisasi adui zake,Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake.
44 Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni.
45 Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote;