41 Nikiunoa upanga wangu wa umeme,Mkono wangu ukishika hukumu,Nitawatoza kisasi adui zangu,Nitawalipa wanaonichukia.
42 Nitailevya mishale yangu kwa damu,Na upanga wangu utakula nyama;Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara,Katika vichwa vya wakuu wa adui.
43 Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake;Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake,Atawatoza kisasi adui zake,Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake.
44 Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni.
45 Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote;
46 akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii.
47 Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.