1 Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake.
2 Akasema,BWANA alitoka Sinai,Akawaondokea kutoka Seiri;Aliangaza katika kilima cha Parani,Akaja Meribath-kadeshi.Upande wa mkono wake wa kuumePalikuwa na sheria ya moto-moto kwao.
3 Hakika awapenda hayo makabila ya watu;Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako;Nao waliketi miguuni pako;Watapokea kila mmoja katika maneno yako.
4 Musa alituagiza torati,Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo.
5 Akawa mfalme katika Yeshuruni,Walipokutanika wakuu wa watu,Makabila yote ya Israeli pamoja.
6 Reubeni na aishi, asife;Lakini watu wake na wawe wachache.
7 Na baraka ya Yuda ni hii; akasema,Isikize, Ee BWANA, sauti ya Yuda,Umlete ndani kwa watu wake;Alijitetea kwa mikono yake;Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake.