20 Na Gadi akamnena,Na abarikiwe amwongezaye Gadi;Yeye hukaa kama simba mke,Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.
21 Akajichagulia sehemu ya kwanza,Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria;Akaja pamoja na wakuu wa watu,Akaitekeleza haki ya BWANA,Na hukumu zake kwa Israeli.
22 Na Dani akamnena,Dani ni mwana-simba,Arukaye kutoka Bashani.
23 Na Naftali akamnena,Ee Naftali, uliyeshiba fadhili,Uliyejawa na baraka ya BWANA;Umiliki magharibi na kusini.
24 Na Asheri akamnena,Na abarikiwe Asheri kwa watoto;Na akubaliwe katika nduguze,Na achovye mguu wake katika mafuta.
25 Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba;Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.
26 Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni,Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie.Na juu ya mawingu katika utukufu wake.