26 Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni,Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie.Na juu ya mawingu katika utukufu wake.
27 Mungu wa milele ndiye makazi yako,Na mikono ya milele i chini yako.Na mbele yako amemsukumia mbali adui;Akasema, Angamiza.
28 Na Israeli anakaa salama,Chemchemi ya Yakobo peke yake,Katika nchi ya ngano na divai;Naam, mbingu zake zadondoza umande.
29 U heri, Israeli.Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA!Ndiye ngao ya msaada wako,Na upanga wa utukufu wako;Na adui zako watajitiisha chini yako,Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.