4 Musa alituagiza torati,Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo.
5 Akawa mfalme katika Yeshuruni,Walipokutanika wakuu wa watu,Makabila yote ya Israeli pamoja.
6 Reubeni na aishi, asife;Lakini watu wake na wawe wachache.
7 Na baraka ya Yuda ni hii; akasema,Isikize, Ee BWANA, sauti ya Yuda,Umlete ndani kwa watu wake;Alijitetea kwa mikono yake;Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake.
8 Akamnena Lawi,Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako,Uliyemjaribu huko Masa;Ukateta naye kwenye maji ya Meriba.
9 Aliyemtaja baba yake na mama yake, Mimi sikumwona;Wala nduguze hakuwakubali;Wala hakuwajua watoto wake mwenyewe;Maana wameliangalia neno lako,Wamelishika agano lako.
10 Watamfundisha Yakobo hukumu zako,Na Israeli torati yako,Wataweka uvumba mbele zako,Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako.