13 Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.
14 Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;
15 kwani BWANA, Mungu wako, aliye katikati yako ni Mungu mwenye wivu; isije ikawaka juu yako hasira ya BWANA, Mungu wako, akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi.
16 Msimjaribu BWANA, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa.
17 Zishikeni kwa bidii sheria za BWANA, Mungu wenu, na mashuhudizo yake, na amri zake alizokuagiza.
18 Nawe fanya yaliyo sawa, na mema, machoni pa BWANA; ili mpate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kuimiliki nchi nzuri BWANA aliyowaapia baba zako,
19 ya kuwa atawasukumia nje adui zako wote mbele yako, kama alivyosema BWANA.