6 nawe mvike kile kilemba kichwani, na ile taji takatifu utaitia katika kile kilemba.
7 Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kutiwa, na kummiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta.
8 Kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu.
9 Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.
10 Kisha utamleta huyo ng’ombe mbele ya hema ya kukutania; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo ng’ombe.
11 Kisha utamchinja huyo ng’ombe mbele ya BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania.
12 Kisha twaa baadhi ya damu ya ng’ombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu.