1 BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
3 Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msiende katika amri zao hao.
4 Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.