26 Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.
27 Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.
28 Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.
29 Usimnajisi binti yako, ili kumfanya awe kahaba; isiwe hiyo nchi kuuandama ukahaba, na nchi kujawa na uovu mkuu.
30 Zishikeni Sabato zangu, mpaheshimu patakatifu pangu; mimi ndimi BWANA.
31 Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
32 Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi BWANA.