33 Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu.
34 Mgeni akaaye pamoja nawe atakuwa kama mzalia kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
35 Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo.
36 Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri.
37 Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi BWANA.