11 wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake;
12 wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake u juu yake; mimi ndimi BWANA.
13 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.
14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.
15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi BWANA nimtakasaye.
16 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
17 Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.