13 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.
14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.
15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi BWANA nimtakasaye.
16 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
17 Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.
18 Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili,
19 au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,