10 vile vile kama yanavyoondolewa katika ng’ombe wa kuchinjwa kwa sadaka za amani; kisha huyo kuhani atayateketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.
11 Kisha ngozi yake ng’ombe, na nyama yake yote, pamoja na kichwa chake, na pamoja na miguu yake, na matumbo yake, na mavi yake,
12 maana, huyo ng’ombe mzima atamchukua nje ya marago hata mahali safi, hapo wamwagapo majivu, naye atamchoma moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo majivu yamwagwapo.
13 Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi, na jambo lenyewe likayafichamania macho ya huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na BWANA, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia;
14 hapo itakapojulikana hiyo dhambi waliyoifanya, ndipo mkutano utatoa ng’ombe mume mchanga awe sadaka ya dhambi, na kumleta mbele ya hema ya kukutania.
15 Kisha wazee wa mkutano wataweka mikono yao kichwani mwake huyo ng’ombe mbele za BWANA;
16 kisha ng’ombe atachinjwa mbele za BWANA. Kisha kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa katika damu ya huyo ng’ombe na kuileta ndani ya hema ya kukutania;