19 Kisha atayaondoa mafuta yake yote na kuyateketeza juu ya madhabahu.
20 Ndivyo atakavyomfanyia huyo ng’ombe; kama alivyomfanyia huyo ng’ombe wa sadaka ya dhambi, atamfanyia na huyu vivyo; naye kuhani atawafanyia upatanisho, nao watasamehewa.
21 Kisha atamchukua huyo ng’ombe nje ya marago, na kumchoma moto vile vile kama alivyomchoma moto ng’ombe wa kwanza; ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mkutano.
22 Mtawala atakapofanya dhambi, na kutenda pasipo kukusudia neno lo lote katika hayo ambayo BWANA, Mungu wake, aliyazuilia yasifanywe, naye amepata hatia;
23 akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya, ataleta mbuzi awe matoleo yake, mume, mkamilifu;
24 kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za BWANA; ni sadaka ya dhambi.
25 Kisha kuhani atatwaa katika damu ya hiyo sadaka ya dhambi kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, nayo damu yake ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya kuteketeza.