4 Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika tena kutelemka gengeni.
5 Kwa sababu ya kosa la Yakobo yametokea haya yote, na kwa sababu ya makosa ya nyumba ya Israeli. Nini kosa la Yakobo? Je, silo Samaria? Na nini mahali pa Yuda palipoinuka? Sipo Yerusalemu?
6 Kwa ajili ya hayo nitafanya Samaria kuwa kama chungu katika shamba, na kama miche ya shamba la mizabibu; nami nitayatupa mawe yake bondeni, nami nitaifunua misingi yake.
7 Na sanamu zake zote za kuchonga zitapondwa-pondwa, na ijara zake zote zitateketezwa kwa moto, na sanamu zake zote nitazifanya ukiwa; kwa kuwa amezikusanya kwa ujira wa kahaba, nazo zitaurudia ujira wa kahaba.
8 Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia,Nitakwenda nimevua nguo, ni uchi;Nitafanya mlio kama wa mbweha,Na maombolezo kama ya mbuni.
9 Kwa maana jeraha zake haziponyekani;Maana msiba umeijilia hata Yuda,Unalifikia lango la watu wangu,Naam, hata Yerusalemu.
10 Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe;Katika Beth-le-Afra ugae-gae mavumbini.