9 Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe.
10 Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana.
11 Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi.
12 Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili.
13 Lea akasema, Ni heri mimi, maana wanawake wataniita heri. Akamwita jina lake Asheri.
14 Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao.
15 Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang’anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao.