1 Jinsi Bwana alivyomfunika binti SayuniKwa wingu katika hasira yake!Ameutupa toka mbinguni hata nchiHuo uzuri wa Israeli;Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yakeKatika siku ya hasira yake.
2 Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo,Wala hakuona huruma;Ameziangusha ngome za binti YudaKatika ghadhabu yake;Amezibomoa hata nchiAmeunajisi ufalme na wakuu wake.
3 Ameikata pembe yote ya IsraeliKatika hasira yake kali;Ameurudisha nyuma mkono wake wa kuumeMbele ya hao adui,Naye amemteketeza Yakobo kama moto uwakao,Ulao pande zote.
4 Ameupinda upinde wake kama adui,Amesimama na mkono wake wa kuume kama mtesi;Naye amewaua hao woteWaliopendeza macho;Katika hema ya binti SayuniAmemimina kani yake kama moto.
5 Bwana amekuwa mfano wa adui,Amemmeza Israeli;Ameyameza majumba yake yote,Ameziharibu ngome zake;Tena amemzidishia binti YudaMatanga na maombolezo.
6 Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu,Kana kwamba ni ya bustani tu;Ameziharibu sikukuu zake;BWANA amezisahauzisha katika SayuniSikukuu za makini na sabato;Naye amewadharau mfalme na kuhaniKatika uchungu wa hasira yake.
7 Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake,Amepachukia patakatifu pake;Amezitia katika mikono ya hao aduiKuta za majumba yake;Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya BWANAKama katika siku ya kusanyiko la makini.