6 Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie,Nitakwenda kwenye mlima wa manemane,Na kwenye kilima cha ubani.
7 Mpenzi wangu, u mzuri pia pia,Wala ndani yako hamna ila.
8 Bibi arusi, njoo pamoja nami toka Lebanoni,Pamoja nami toka Lebanoni.Shuka kutoka kilele cha Amana,Kutoka vilele vya Seniri na Hermoni;Kutoka mapangoni mwa simba,Kutoka milimani mwa chui.
9 Umenishangaza moyo, umbu langu,Bibi arusi, umenishangaza moyo,Kwa mtupo mmoja wa macho yako,Kwa mkufu mmoja wa shingo yako.
10 Jinsi zilivyo nzuri pambaja zako, umbu langu,Bibi arusi, ni nzuri kupita divai;Na harufu ya marhamu yakoYapita manukato ya kila namna.
11 Bibi arusi, midomo yako yadondoza asali,Asali na maziwa vi chini ya ulimi wako;Na harufu ya mavazi yakoNi kama harufu ya Lebanoni.
12 Bustani iliyofungwa ni umbu langu, bibi arusi,Kijito kilichofungwa, chemchemi iliyotiwa muhuri.