9 Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi, kazi ya stadi na ya mikono ya mfua dhahabu; mavazi yao ni rangi ya samawi na urujuani; hayo yote ni kazi ya mafundi yao.
10 Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli;Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele;Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka,Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.
11 Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu.
12 Ameiumba dunia kwa uweza wake,Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake,Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
13 Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni,Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi;Huifanyia mvua umeme,Huutoa upepo katika hazina zake.
14 Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa;Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga;Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo,Wala hamna pumzi ndani yake.
15 Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu;Wakati wa kujiliwa kwao watapotea.