1 BWANA akaniambia hivi, Enenda, ukajinunulie mshipi wa kitani, ukajivike viuno, wala usiutie majini.
2 Basi nikanunua mshipi sawasawa na neno la BWANA, nikajivika viunoni.
3 Nalo neno la BWANA likanijia mara ya pili, kusema,
4 Twaa mshipi ule ulioununua, ulio viunoni mwako, kisha ondoka, enenda mpaka mto Frati, ukaufiche huko katika pango la jabali.
5 Basi nikaenda, nikauficha karibu na mto Frati, kama BWANA alivyoniamuru.