24 Kwa sababu hiyo nitawatawanya, kama makapi yapitayo, kwa upepo wa jangwani.
25 Hiyo ndiyo kura yako, fungu lako ulilopimiwa na mimi, asema BWANA; kwa kuwa umenisahau, na kuutumainia uongo.
26 Kwa ajili ya hayo, mimi nami nitayafunua marinda yako mbele ya uso wako, na aibu yako itaonekana.
27 Nimeona machukizo yako, naam, uzinifu wako, na ubembe wako, na uasherati wa ukahaba wako, juu ya milima katika mashamba. Ole wako, Ee Yerusalemu! Hutaki kutakaswa; mambo hayo yataendelea hata lini?