1 Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao, na katika pembe za madhabahu zenu;
2 na wakati huo watoto wao wazikumbuka madhabahu zao, na maashera yao, karibu na miti yenye majani mabichi juu ya milima mirefu.
3 Ee mlima wangu wa uwandani, nitatoa mali zako na hazina zako zote ziwe nyara, na mahali pako palipoinuka, kwa sababu ya dhambi, katika mipaka yako yote.
4 Nawe, naam, wewe nafsi yako, utaachana na urithi wako niliokupa; nami nitakulazimisha kuwatumikia adui zako katika nchi usiyoijua; maana umewasha moto katika hasira yangu, utakaowaka milele.
5 BWANA asema hivi,Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu,Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yakeNa moyoni mwake amemwacha BWANA.
6 Maana atakuwa kama fukara nyikani,Hataona yatakapotokea mema;Bali atakaa jangwani palipo ukame,Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA,Ambaye BWANA ni tumaini lake.