4 Nawe, naam, wewe nafsi yako, utaachana na urithi wako niliokupa; nami nitakulazimisha kuwatumikia adui zako katika nchi usiyoijua; maana umewasha moto katika hasira yangu, utakaowaka milele.
5 BWANA asema hivi,Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu,Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yakeNa moyoni mwake amemwacha BWANA.
6 Maana atakuwa kama fukara nyikani,Hataona yatakapotokea mema;Bali atakaa jangwani palipo ukame,Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA,Ambaye BWANA ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji,Uenezao mizizi yake karibu na mto;Hautaona hofu wakati wa hari ujapo,Bali jani lake litakuwa bichi;Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua,Wala hautaacha kuzaa matunda.
9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
10 Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.