11 Na katika habari za nyumba ya mfalme wa Yuda, lisikieni neno la BWANA,
12 Ee nyumba ya Daudi, BWANA asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu ye yote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
13 Tazama, mimi ni juu yako, Ewe ukaaye bondeni, na kwenye jabali la uwandani, asema BWANA ninyi mnaosema, Ni nani atakayeshuka apigane nasi? Au, Ni nani atakayeingia katika makao yetu?
14 Nami nitawaadhibu kwa kadiri ya matunda ya matendo yenu, asema BWANA; nami nitawasha moto katika msitu wake, nao utateketeza vitu vyote viuzungukavyo.