37 Nawe utamwambia nabii hivi, BWANA amekujibu nini? Na, BWANA amesemaje?
38 Lakini mkisema, Mzigo wa BWANA, basi, BWANA asema hivi, Kwa sababu mwasema neno hili, “Mzigo wa BWANA”; nami nimemtuma mtu kwenu kusema, Msiseme, “Mzigo wa BWANA”;
39 basi, kwa hiyo angalieni, nitawasahau ninyi kabisa, nami nitawatupilia mbali, pamoja na mji huu niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke mbele za uso wangu;
40 nami nitaleta juu yenu aibu ya milele, na fedheha ya daima, ambayo haitasahauliwa.