1 Ikawa Yeremia alipokwisha kuwaambia watu wote maneno yote ya BWANA, Mungu wao, ambayo BWANA, Mungu wao, amemtuma kwao, yaani, maneno hayo yote,
2 ndipo Azaria, mwana wa Hoshaya, na Yohana mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakanena, wakimwambia Yeremia, Unasema uongo; BWANA, Mungu wetu, hakukutuma useme, Msiende Misri kukaa huko;
3 bali Baruku, mwana wa Neria, akushawishi kinyume chetu, ili kututia katika mikono ya Wakaldayo, ili watuue, na kutuchukua mateka mpaka Babeli.
4 Basi Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi, na watu wote hawakuitii sauti ya BWANA, kwamba wakae katika nchi ya Yuda.