1 Habari za wana wa Amoni. BWANA asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake?
2 Basi, kwa sababu hiyo, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakaposikizisha mshindo wa vita juu ya Raba, mji wa Amoni, nao utakuwa magofu ya ukiwa, na binti zake watateketezwa kwa moto; ndipo Israeli watawamiliki wao waliokuwa wakimmiliki, asema BWANA.
3 Piga yowe, Ee Heshboni,Kwa maana Ai umeangamizwa;Lieni, enyi binti za Raba,Mjivike nguo za magunia;Ombolezeni, mkipiga mbioHuko na huko kati ya maboma;Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa,Makuhani wake na wakuu wake pamoja.
4 Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijilia?
5 Tazama, nitaleta hofu juu yako, asema Bwana, BWANA wa majeshi, itakayotoka kwa wote wakuzungukao; nanyi mtafukuzwa nje, kila mtu mbali kabisa, wala hapana mtu wa kuwakusanya wapoteao.