50 Ninyi mliojiepusha na upanga,Enendeni zenu, msisimame;Mkumbukeni BWANA tokea mbali,Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.
51 Twaona haya kwa kuwa tumesikia mashutumu;Fedheha imetufunikiza nyuso zetu;Kwa sababu wageni wamepaingiaPatakatifu pa nyumba ya BWANA.
52 Kwa sababu hiyo siku zinakuja, asema BWANA, nitakapozihukumu sanamu zake; na katika nchi yake yote waliojeruhiwa wataugua.
53 Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.
54 Sauti ya kilio kutoka Babeli,Na ya uangamivu mkuu toka nchi ya Wakaldayo!
55 Maana BWANA amwangamiza Babeli,Na kuikomesha sauti kuu ndani yake;Na mawimbi yake yavuma kama maji mengi,Mshindo wa sauti zao wafanya makelele;
56 Kwa maana mwenye kuangamiza amefika kwake;Naam, amefika Babeli;Na mashujaa wake wametwaliwa;Pinde zao zimevunjika kabisa;Maana BWANA ni Mungu wa kisasi;Hakika yake yeye atalipa.