1 Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, kusema,
2 Simama langoni pa nyumba ya BWANA, ukatangaze hapo neno hili, ukisema, Sikilizeni neno la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mnaoingia katika malango haya ili kumwabudu BWANA.
3 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tengenezeni njia zenu, na matendo yenu, nami nitawakalisha ninyi mahali hapa.
4 Msitumainie maneno ya uongo, mkisema, Hekalu la BWANA, Hekalu la BWANA, Hekalu la BWANA ndiyo haya.
5 Maana kama mkitengeneza kabisa njia zenu na matendo yenu; kama mkihukumu hukumu ya haki kati ya mtu na jirani yake;