1 Ifungue milango yako, Ee Lebanoni,Ili moto uiteketeze mierezi yako.
2 Piga yowe, msunobari, maana mwerezi umeanguka,Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika;Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani,Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.
3 Sauti ya wachungaji, ya uchungu mwingi!Kwa maana utukufu wao umeharibika;Sauti ya ngurumo ya wana-simba!Kwa maana kiburi cha Yordani kimeharibika.
4 BWANA, Mungu wangu, alisema hivi, Lilishe kundi la machinjo,
5 ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe BWANA, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.
6 Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema BWANA; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa mikononi mwao.