38 Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia:“Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu?Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?”
39 Hivyo hawakuweza kuamini, kwani Isaya alisema tena:
40 “Mungu ameyapofusha macho yao,amezipumbaza akili zao;wasione kwa macho yao,wasielewe kwa akili zao;wala wasinigeukie, asema Bwana,ili nipate kuwaponya.”
41 Isaya alisema maneno haya kwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasema habari zake.
42 Hata hivyo, wengi wa viongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuogopa kwamba watatengwa na sunagogi.
43 Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu.
44 Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, “Mtu anayeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma.