20 Wana wa Yoktani walikuwa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
21 Hadoramu, Uzali, Dikla,
22 Obali, Abimaeli, Sheba,
23 Ofiri, Havila na Yobabu. Hao watu ni wana wa Yoktani.
24 Ukoo wa Abrahamu kutokea Shemu ni kama ifuatavyo: Shemu alimzaa Arpaksadi, naye Arpaksadi akamzaa Shela.
25 Shela akamzaa Eberi, Eberi akamzaa Pelegi, Pelegi akamzaa Reu;
26 Reu akamzaa Serugi, Serugi akamzaa Nahori, Nahori akamzaa Tera,