24 Benaya, mwana wa Yehoyada alifanya mambo haya, akajipatia jina miongoni mwa wale mashujaa watatu.
25 Basi, akawa mashuhuri kati ya wale mashujaa thelathini, ingawa hakuwa shujaa kama wale mashujaa watatu. Na Daudi akampa cheo cha mkuu wa walinzi wake binafsi.
26 Wanajeshi mashujaa wa Daudi walikuwa: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethlehemu,
27 Shamothi Mharodi, Helesi Mpeloni,
28 Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa, Abiezeri Mwanathothi;
29 Sibekai Mhushathi; Ilai Mwahohi;
30 Maharai Mnetofathi; Heledi, mwana wa Baana Mnetofathi;