9 Kiongozi wao mkuu alikuwa Ezeri, wa pili Obadia, wa tatu Eliabu,
10 wa nne Mishmana, wa tano Yeremia,
11 wa sita Atai, wa saba Elieli,
12 wa nane Yohanani, wa tisa Elsabadi,
13 wa kumi Yeremia, na wa kumi na moja Makbanai.
14 Wagadi hao, walikuwa maofisa wa jeshi. Kulingana na vyeo vyao, mdogo alisimamia kikosi cha wanajeshi 100, na mkubwa alisimamia kikosi cha wanajeshi 1,000.
15 Hawa ndio watu waliovuka mto Yordani mnamo mwezi wa kwanza, mto ulipokuwa umefurika pande zote na kuwatawanya watu mashariki na magharibi ya mto.