10 Wana wa Shimei walikuwa viongozi wanne: Yahathi, Zina, Yeushi na Beria.
11 Yahathi ndiye aliyekuwa mkuu wao, akifuatiwa na Ziza. Lakini Yeushi na Beria, kwa vile hawakuwa na wana wengi, walichukuliwa na ukoo mmoja.
12 Wana wa Kohathi walikuwa wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
13 Wana wa Amramu walikuwa Aroni na Mose. Aroni aliteuliwa awe akiweka wakfu vyombo vitakatifu kabisa, pia wazawa wake daima wafukizie ubani mbele za Mwenyezi-Mungu, wakimtumikia na kuwabariki watu katika jina la Mwenyezi-Mungu milele.
14 Lakini wana wa Mose, mtu wa Mungu, hutajwa miongoni mwa kabila la Lawi.
15 Wana wa Mose walikuwa Gershomu na Eliezeri.
16 Aliyekuwa mkuu miongoni mwa wana wa Gershomu ni Shebueli.