16 Aliyekuwa mkuu miongoni mwa wana wa Gershomu ni Shebueli.
17 Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu; Rehabia, naye alikuwa kiongozi. Lakini Rehabia alikuwa na wana wengi sana.
18 Ishari alimzaa Shelomithi, kiongozi wa kabila zima.
19 Wana wa Hebroni walikuwa wanne: Mkuu wao alikuwa Yeria, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli na wa nne Yekameamu.
20 Wana wa Uzieli walikuwa wawili: Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.
21 Merari alikuwa na wana wawili: Mali na Mushi. Wana wa Mali walikuwa wawili: Eleazari na Kishi.
22 Eleazari alifariki bila kupata mtoto wa kiume, ila mabinti tu. Mabinti hao waliolewa na binamu zao, wana wa Kishi.