2 Mfalme Daudi aliwakusanya wakuu wote wa Israeli, makuhani na Walawi.
3 Walawi wote wanaume wenye umri wa miaka thelathini na zaidi, wakahesabiwa. Jumla yao ilikuwa 38,000.
4 Hao, Daudi aliwagawanya: 24,000 kati yao wawe wasimamizi wa kazi ya nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, 6,000 wawe maofisa na waamuzi,
5 4,000 wawe mabawabu, na 4,000 wawe waimbaji, wakimsifu Mwenyezi-Mungu kwa ala za muziki alizotengeneza mfalme mwenyewe kwa madhumuni hayo.
6 Daudi aliwagawanya Walawi katika makundi matatu kulingana na koo za kabila la Lawi: Ukoo wa Gershoni, ukoo wa Kohathi na ukoo wa Merari.
7 Wana wa Gershoni walikuwa wawili: Ladani na Shimei.
8 Ladani alikuwa na wana watatu: Yehieli mkuu wao, Zethamu na Yoeli.