6 Daudi aliwagawanya Walawi katika makundi matatu kulingana na koo za kabila la Lawi: Ukoo wa Gershoni, ukoo wa Kohathi na ukoo wa Merari.
7 Wana wa Gershoni walikuwa wawili: Ladani na Shimei.
8 Ladani alikuwa na wana watatu: Yehieli mkuu wao, Zethamu na Yoeli.
9 Wana wa Shimei walikuwa watatu: Shelomithi, Hazieli na Harani. Hawa walikuwa viongozi wa ukoo wa Ladani.
10 Wana wa Shimei walikuwa viongozi wanne: Yahathi, Zina, Yeushi na Beria.
11 Yahathi ndiye aliyekuwa mkuu wao, akifuatiwa na Ziza. Lakini Yeushi na Beria, kwa vile hawakuwa na wana wengi, walichukuliwa na ukoo mmoja.
12 Wana wa Kohathi walikuwa wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.